Mtoto wa Mama by Adam Shafi ni riwaya inayotoa taswira ya maisha ya familia ya mzazi mmoja Zamda na mtoto wake, saburi. wote wamepotelewa, zamda na mume wake Sahuri na saburi na baba yake. Hawajui alipo. Hawajui kama yu hai au kafa.
Walipojua, tayari jalala, mtawala mkuu wa nchi alikuwa tayari ammkuhukumu Shauri adhabu ya kifo kwa kunyongwa hadharani. Kabla ya hukumu hiyo kutekelezwa, shauri tayari kitanzi kimemzunguka rohonzi.
Saburi, mwanwe shauri na mahamali wenzake wa mbele ya njia kuu wanawavamia walinzi wa jela na kuwanganganya silaha. Sasa jalala yu mashakani, na shauri yumo matatani zaidi. Nani atapona? saburi na nguvu zake na maarifa aliyoyapata mble ya njia kuu vitamwezesha kulizipiza kisasi hiki au atabaki kuwa mtoto wa mama tu?
Baada ya kisa, saburi, mama yake na wahisani wao wanakimbilia kisiwa cha majini ambako wanapokelewa kwa huruma na ukarimu.
Mtoto wa mama ni riwaya ambayo ukianza kuisoma itakugandisha hapo hapo ulipokaa mpaka uimalize.
Reviews
There are no reviews yet.