Isimujamii kwa Wanafunzi wa Kiswahili ni kazi inayonuia kikidhi baadhi ya mahitaji ya kimsingi ya usomaji wa kiswahil katika shule za upili, vyuo vya ualimu, vyuo vikuu na taasisi zingine zinazoshughulika lugha na mawasiliano. Pamoja na kufundishwa katika viwango mbalimabli vya elimu, Isimujamii ni taaluma inayoonekana kuingiana na mahitaji ya taaluma zinazotumikiwa maarifa juu ya mfumo wa lugha. Isimujamii humulika jinsi vigezo mbalimabali vya kijamii vinavyoathiri matumizi ya lugha.
Lengo kuu la Isimujamii kwa wanafunzi wa kiswahili ni kusisimua uelewa na uthumani wa vigezo muhimu vya matumizi ya lugha, pamoja na kuhamasisha wasomi kwa utafiti wa masuala nyeti yanayohusu uwiano wa lugha ya jamii. Ili kudhibiti lengo, masomo yote ambayo yameunda kitabu kamili yamewasilishwa kwa maelezo na uadihirishi wenye uangavu. Uangavu mahususi umenuiwa kurahisha usomaji bila kubatilisha uzito wa dhana na hoja msingi.
Reviews
There are no reviews yet.